Kisa Picha ya Eric Omondi, Harmonize Awatolea Uvivu Waandaaji wa Tamasha la Africa Moja


Msanii @harmonize_tz ameonesha wazi kutofurahishwa na poster ya tamasha la Afrika Moja linalotarajiwa kufanyika nchini Kenya mwishoni mwa mwezi huu, Aprili 30.

Boss huyo wa Konde Gang, kupitia insta story yake ameeleza kwamba kitendo walichokifanya Waandaaji wa tamasha hilo sio cha kiungwana kufuatia picha yake ikionekana kubwa huku picha ya mchekeshaji nyota nchini humo @ericomondi ikiwa ndogo.


Harmonize ameeleza kuwa Omondi ni mkubwa kwake kiumri na kisanaa pia, akidai kuwa picha hiyo imewekwa kama Omondi anakuja kufanya usafi tu katika uwanja wa KICC ambapo tamasha hilo litafanyika. "Sisi ni wamoja, hatuwezi kukuzana kwa kuwakandamiza wengine" - ameeleza.

Aidha, Harmonize awataka waandaaji wa tamasha hilo watengeneze poster nyingine ili aweze kupost kwenye uso wa ukurasa wake (feed).


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad