Kisasi cha Ukraine: Raia Wawalisha Wanajeshi wa Urusi Mandazi yenye Sumu



Wanajeshi wa Urusi karibu na Izium mji mkuu wa Kharkiv wamedaiwa kulishwa sumu na raia wa Ukraine ambao waliwapa wanajeshi hao chakula
Wanajeshi wawili wanadaiwa kufariki dunia baada ya kula maandazi mawili yaliyokuwa yamejazwa au mikate ndogo na askari wengine 28 wamelazwa hospitalini wakiwa na 'maumivu makali'
Kulingana na ripoti za ziada, mamia ya wanajeshi wengine wa Urusi wamepigwa risasi baada ya kunywa pombe yenye sumu iliyotolewa na wakaazi
Raia wa Ukraine wanakabiliana na wavamizi wa Urusi kwa kutia sumu kwenye chakula katika juhudi za kuhujumu ushambulizi wa wanajeshi hao.


Wanajeshi wa Urusi wanadaiwa kulishwa sumu na raia wa Ukraine Picha: The Asahi Shimbun.
Yamkini wanajeshi wawili wa Urusi wamfariki huku wengine 28 zaidi wakiugua baada ya kula chakula walichopewa na raia wa Ukraine.

Wanajeshi walioathirika walikuwa wa kitengo cha 3rd Motor Rifle Division.

Kulingana na ripoti ya Idara Ujasusi ya Ukraine, wanajeshi wawili walifariki papo hapo mara baada ya kula mandazi au mikate ndogo.


 
Huffington Post iliripoti kwamba sumu na vifo havijathibitishwa kikamilifu na haijulikani ni sumu gani iliyotumika.

Pombe yenye sumu
Gazeti la Daily Mail pia liliripoti juu ya tukio lililotokea karibu na mji wa Izium mkabala na Kharkiv. Wakazi wa Izium wanadaiwa kuwapa askari hao vikapu vya chakula.

Kulingana na ripoti mamia ya wanajeshi wa Urusi wanaugua 'ugonjwa mbaya' baada ya kudaiwa kunywa pombe yenye sumu iliyotolewa na raia.


Kyiv inaripotiwa kupata mashambulizi makubwa ya Urusi mashariki mwa nchi hiyo ambapo wanajeshi wa Putin walikuwa wakitayarisha kwa operesheni.

AFP iliripoti kuwa mamlaka ya Ukraine ilisema zaidi ya miili 1,200 imepatikana katika eneo hilo hadi sasa na kwamba wanawazia kesi dhidi ya "washukiwa 500", akiwemo Putin na maafisa wengine wakuu wa Urusi.

"Wanaweza kutumia hata makombora zaidi dhidi yetu... Lakini tunajiandaa kwa matendo yao. Tutajibu," alisema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Vita kwa raia
Lakini wanajeshi wa Urusi wanaendeleza mashambulizi dhidi ya raia wa Ukraine. Mwishoni mwa juma, watu 11 waliuawa, akiwemo mtoto wa miaka saba.

"Jeshi la Urusi linaendelea kupigana vita na raia kutokana na ukosefu wa ushindi mbele," gavana wa eneo la kaskazini mashariki Oleg Synegubov alisema kwenye Telegram.

Wakati huo huo, kiongozi wa Austria alikutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin mnamo Jumatatu, Aprili 11, akiwa mtu wa kwanza Uropa kuzuru Moscow tangu vita kuanza.

Karl Nehammer anatarajiwa kuibua madai ya uhalifu wa kivita katika maeneo yaliyoharibiwa karibu na Kyiv ambayo yalikuwa chini ya uvamizi wa Urusi, ukiwemo mji wa Bucha
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad