KIUNGO wa klabu ya Simba Clatous Chama amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwezi Machi kufuatia kuonesha kiwango bora akiwa na kikosi cha klabu ya Simba ambao ndio mabingwa watetezi wa taji hilo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Chama ameshinda tuzo hiyo mara baada ya kumshinda mshambuliaji hatari wa klabu ya Yanga Fiston Mayele na Frank Kahole wa Mtibwa Sugar ambao aliingia nao fainali.
Mchezaji huyo ambaye ambaye alirejea ndani ya klabu ya Simba kwenye dirisha dogo la usajili, ndani ya Mwezi Machi alifanikiwa kuisadia klabu yake ya Simba kuibuka na ushindi katika michezo miwili na kufunga mabao mawili.
Fiston Mayele, mshambuliaji wa Yanga
Tuzo hiyo ya Chama inakluwa tuzo ya kwanza ya mchezaji bora wa Ligi kutoka ndani ya klabu ya Simba, toka kuanza kwa msimu mpya wa mashindano 2021/2022.
Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa saba kutwaa tuzso hiyo toka kuanza kwa msimu mpya, huku wachezaji wengine waliofanikiwa kutwaa tuzo hiyo ni Saido Ntibazonkiza (Februari) na Fiston Mayele (Januari) wote wa Yanga, Reliants Lusajo wa Namungo (Desemba), Jeremiah Juma wa Prisons (Novemba), Feisal Salum wa Yanga (Oktoba) na Vitalis Mayanga wa Polisi Tanzania (Septemba).