Kocha wa Chelsea Akiri Mechi ya Marudiano dhidi ya Real Madrid Imeshaisha



TUMESHATOLEWA. Ndivyo alivyosema Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel, baada ya kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Real Madrid kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi Jumatano nyumbani Stamford Bridge.

Mabao matatu ‘hat trick’ ya Karim Benzema yameipa Real Madrid faida kuelekea mchezo wa marudiano Jumanne ijayo jijini Madrid.

Na Tuchel alipoulizwa kama gemu bado ipo, alijibu: “Hapana, mchezo umeshaisha.


                                                       Kikosi cha Real Madrid
“Tunatakiwa kukitafuta kiwango chetu kwa sababu tangu mapumziko ya kimataifa (tumepotea). Naogopa zaidi mechi ya Southampton wikiendi hii.”


 
Aliongeza: “Huwezi kutarajia matokeo kwa kiwango cha namna hii. Tunahitaji mabao matatu na mara ngapi hili limetokea? Tuwe wakweli.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad