Kwa mara ya kwanza, Mwanadada Rihanna ameingia kwenye orodha ya mabilionea inayotolewa na Jarida la Forbes kila mwaka. Riri ametajwa kwenye nafasi ya 1,729 akiwa na utajiri wa ($1.7B) sawa na zaidi ya TSh. Trilioni 3.9
Anatajwa kuwa Bilionea wa kwanza toka visiwani Barbados, na mwanamke tajiri zaidi kwa upande wa wanamuziki wa Kike duniani.