Makumi ya vijana wa Ethiopia wanaendelea kukusanyika katika ubalozi wa Urusi mji mkuu Addis Ababa, Jumanne kufuatia uvumi wa kuajiriwa kwa wanajeshi kupigana nchini Ukraine.
Lakini msemaji wa ubalozi huo, Maria Chernukhina, alisema hakuna uajiri unaofanywa nchini Ethiopia.
Alisema watu hao walikuwa wanaonyesha mshikamano na Urusi
"Tuna wageni wengi katika ubalozi huu wanaokuja kuunga mkono Urusi," aliambia BBC.
"Baadhi yao wanatuambia wako tayari kusaidia kwa njia yoyote wanayoweza. Lakini sisi sio wakala wa kuajiri," Bi Chernukhina aliongeza.
Baathi ya vijana hao wa Ethiopia katika ubalozi huo walionekana wakiwa na hati zao za kibinafsi.
Kijana aliyekuwa akisubiri mlangoni aliambia BBC kwamba anatafuta mshahara mzuri kama mwanajeshi au kuajiriwa katika kazi nyingine yoyote inayopatikana.Pia napenda Urusi," alisema.
Wengine walisema wamesikia fununu za mishahara mikubwa nchini Urusi.
Ethiopia ilikuwa miongoni mwa nchi zilizokosa kikao cha Umoja wa Mataifa cha kupigia kura azimio kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.