Lusinde Aliamsha Sakata la Mafuta Bungeni



Mbunge wa Mvumi (CCM) Livingstone Lusinde akizungumza bungeni leo Jumanne Aprili 12, 2022. Picha na Said Khamis
By Sharon Sauwa
Dodoma. Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde amesema ni hatari kama nchi haina hifadhi ya mafuta na wabunge wanaendelea kudanganyana ndani ya Bunge kwamba nchi iko salama.

Lusinde ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 12, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu 2022/2023.

Lusinde amesema hali ni mbaya sana mitaani hawawezi kufanya kama hawaoni.

Amesema inapotokea njaa kubwa Serikali wanafungua maghala yake ili kushusha bei na hivyo kupunguza makali.


“Vipi Serikali haifungui maghala ya mafuta ya Serikali? Kama hatuna je ni kwanini tusiwe na magahala makubwa ya Serikali ikitokea hali kama hii Serikali inafungua maghala yake inasawazisha mambo yanakaa sawa,”amesema.

Hata hivyo, Mbunge wa Sengerema (CCM), Hamis Tabasamu amempa taarifa kuwa Serikali inayo maghala ya mafuta yenye ubia na Kampuni ya Puma na pia kwenye Tiper wana ghala la kuhifadhi mafuta lita milioni 80.

Akiendelea kuchangia Lusinde amesema kama ni hivyo basi Serikali ifungulie mafuta hayo kisha ishushe.


Mbunge wa Mlalo (CCM) Rashid Shangazi apia amempa taarifa Lusinde kuwa kuna maghala lakini mafuta yaliyopo si ya kwake.

Akiendelea kuchangia Lusinde amesema kama ni kweli, nchi ina mtihani mkubwa sana na kwamba kama imetokea shida, hayo mafuta watayatoa wapi?

“Ni jambo kubwa sana ni suala la usalama wa nchi, hatari kubwa, ni tatizo kubwa tupange bajeti ili tuwe na hifadhi ya Serikali,”amesema.

Hata hivyo, Mbunge wa Muleba Kaskazini (CCM) Charles Mwijage alimpa taarifa Lusinde kuwa kutokana na udhibiti wa mafuta nchi iko salama.


Akiendelea kuchangia Lusinde amesema jambo hilo ni kubwa na kutaka wasiliongelee kwa lugha hiyo.

Amesema vijijini huko lita ya mafuta ya petroli ni sh 4000 na kuhoji nani atakubali kumkimbiza mgonjwa hospitali na magari ya wagonjwa ya Watanzania ni pikipiki.

Ametaka wabunge wazungumze kwa ukubwa wake.

Mchango huo ulimwamsha Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amesema ni kweli jambo hilo ni kubwa na kwamba Serikali inafuatilia kwa umakini mkubwa.


Amesema kuwa Serikali ina mpango wakuweka akiba ya kutosha ya mafuta ambapo wataweza kusambaza pia kwa nchi jirani.

Kuhusu kinachoendelea hivi sasa, Dk Mwigulu amesema wanaangalia jinsi ya kuchomoa fedha kwenye fedha za matumizi ya kawaida zinazokwenda katika taasisi za umma ikiwemo Mamlaka ya Uthibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na Shirika la Viwango Nchini (TBS).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad