Madiwani Wamng’oa Meya Moshi, yeye Aondoka kwa Bodaboda



HATIMAYE Bazara la Madiwani Manispaa ya Moshi Mjini Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania limemng’oa Meya wao, Juma Raibu kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye, baada ya kumtuhuma kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Raibu ameng’olewa leo Jumatatu, tarehe 11 Aprili 2022 katika kikao cha baraza hilo ambapo kati ya madiwani 28 waliopiga kura, zilizomkataa 18 sawa na asilimia 64.3 na 10 zikiwa upande wake sawa na asilimia 35.7.

Miongoni mwa tuhuma hizo ni kutumia nafasi yake vibaya na kwenda kushiriki sherehe ya kijana anayedaiwa kuwa na mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja ‘mashago.’

Tuhuma zingine ni, kuhamisha fedha kutoka kituo cha afya Kaloni na kupeleka Pasua bila kufuata za vikao pamoja na kutuhumiwa kula rushwa na kuruhusu ujenzi holela katikati ya mji.


Aidha, Raibu anatuhumiwa kuwakashfu vibaya madiwani wenzake kwamba hawajui lolote.

Mara baada ya kumaliza kupiga kura na matokeo kutangazwa na naibu meya, Stuart Nkinda atakuwa akikaimu nafasi ya meya hadi baadaye, baraza liliahirishwa.

Raibu aliondoka katika viwanja vya manispaa kwa usafiri wa bodaboda huku wananchi waliokuwemo wakishangilia.



Juma Raibu, alipokuwa Meya wa Manispaa ya Moshi Mjini
Katika ujumbe wake aliouandika kwenye status yake ya simu amesema “Rasmi leo mimi siyo meya wa manispaa ya Moshi. Mungu awajalie wote tulioshirikiana katika mambo yote.”

Sherehe hiyo ya siku ya kuzaliwa ya moja ya shoga, ilifanyika tarehe 11 Februari 2022 katika ukumbi wa klabu moja iliyopo kata ya Bondeni, Manispaa ya Moshi ambako Juma alihudhuria kama mgeni rasmi.

Inaelezwa shoga huyo aliyekuwa na wenzake, waliamua kumualika Raibu ili kada hiyo ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, iweze kutambulika kwani wanapata taabu kutambuliwa na mamlaka za serikali.

Kitendo hicho kiliwakwaza watu mbalimbali wakiwemo Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mkoa waKilimanjaro waliokiandikia barua Chama Cha Mapinduzi (CCM), kulaani tukio hilo na kutaka hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya kiongozi huyo.


Mbali na Bakwata, ndani ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, zilidai kuwa kitendo hicho kimewakasilisha madiwani wengi wa CCM na kumtaka kujiuzulu ili kulinda heshima ya chama chake pamoja na Baraza zima la Madiwani.

Tayari kamati za siasa za wilaya na mkoa wa Kilimanjaro ulimhoji na kumjadili na kupeleka mapendekezo makao makuu ya kutaka achukuliwe hatua ikiwemo kuvuliwa umeya na kuwekwa chini ya uangalizi wa kiezi 12 kutokana na kitendo hicho walichodai kimekidhalilisha.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad