Majizo Afunguka Kuhusu Tuzo za Mziki Tanzania "Kabla ya Kusema Tunawaza Tuzo za Kimataifa, Tuzipe Heshima za Kwetu"




Tuliokaa kwenye hii game kwa miaka mingi tunafahamu jinsi ambavyo watu walihangaika kuja na tuzo. ‘Kili Music Award’ zilikuwa tuzo zetu kubwa zaidi, na japo zilikuwa na madhaifu mengi lakini atakuwa mtu wa hovyo sana atakayeshindwa kutambua mchango wa tuzo zile kwenye muziki wetu. Sitaki tuanze kutajana majina hapa ili mkumbuke ni wasanii wangapi majina yao yalivuma zaidi baada ya wao kupata tuzo nyingi za Kili?, hazikuwa tuzo za Kimataifa, ni za HAPA NDANI. Angalau kumbukeni jinsi ambavyo tuzo zilichangamsha game na kufanya watu watoe kazi kali sana.
.
Baada ya muda mrefu wa sisi kutamani tuzo, Serikali yetu sikivu chini ya Wizara inayosimamia Sanaa imetuletea Tuzo za Muziki Tanzania. Ni kichekesho cha mwaka kusikia kuna wasanii wametukana tuzo hizi na kusema sio lolote. Wamebeza jitihada hizi za Serikali na wadau wengine wa Muziki.
.
Hebu tuache ubinafsi. Sisi ambao tuzo zilitusaidia kujenga majina yetu na kazi zetu leo tunataka kuaminisha watu kwamba tuzo za Tanzania sio kitu chochote?. Ni kweli zina madhaifu, kama ambavyo tuzo zote Duniani hupata malalamiko, sio ajabu hizi zetu kulalamikiwa.

Lakini mnapojitoa kwenye tuzo au mnapogomea tuzo na kuzikejeli, wazeni faida ambazo hizi tuzo zinaweza kuleta. Wazeni kuhusu wasanii ambao zitawajenga, wazeni kuhusu wengi ambao tuzo hizi zitakuwa sherehe kwao na chachu ya wao kutengeneza kazi bora zaidi. Kwa kufanya hivyo mtaisidia ‘Industry’, kabla ya kusema tunawaza tuzo za Kimataifa, tuzipe heshima za kwetu, tuwaze pia kundi kubwa la wanamuziki ambao bado wanahitaji hizi tuzo.
.
Baada ya kusema hayo naishukuru tena Wizara inayosimamia sanaa, Waziri Mchengerwa, Katibu Mkuu @dktabbasi na watendaji wote kwa kitu hiki chema. Yes makosa yapo, Ila ni vyema tumeanza tutarekebisha.
.
Pongezi wasanii wote walioshiriki. Mshinde au msishinde ninyi ni WASHINDI.

Tuzidi kushirikiana katika kuupa nguvu muziki wetu, tushirikiane kuzipa nguvu hizi tuzo na mengine yote yenye faida kwa muziki wetu. Tuache roho za korosho kujiwaza mmoja mmoja, tuwaze Industry yote na penye makosa tukosoe tukiwa na nia ya dhati ya kujenga.

Kesho tukutane kwenye #TanzaniaMusicAwards

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad