Malkia Elizabeth ll wa Uingereza leo amefikisha umri wa miaka 96 na mwaka huu anakuwa Muingereza wa kwanza kufikisha miaka 70 akiwa katika kiti cha umalkia.
Amekua Malkia wa taifa la Uingereza tangu Februari 6, 1952 akiwa na umri wa miaka 25.
Fahamu, picha hii (pichani) ambayo haijawekwa tarehe, imetolewa na The Royal Windsor Horse Show Aprili 20, 2022 inamuonyesha malkia huyo akiwa na farasi wawili, Bybeck Nightingale (kulia) na Bybeck Katie (kushoto), kuadhimisha mwaka wa 96 tangu azaliwe.
✍️: @omaryramsey