Mamlaka ya Dawa "Mauzo ya Dawa za Nguvu za Kiume yapo Juu"



Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imesema tafiti za hivi karibuni zimethibitisha kuwa dawa za kuongeza nguvu za kiume zinaongoza kuuzwa katika maduka ya dawa nchini.

Akizungumza katika kikao kazi cha Wahariri wa habari na TMDA jijini Mbeya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Adam Fimbo amesema dawa inayofuata kwa kununuliwa zaidi ni ya kuzuia kushika mimba maarufu P2.

Hata hivyo, Fimbo amesema licha ya dawa hizo kuuzwa sana, watumiaji wake wanatumia kinyemela na siri kubwa bila ushauri wa daktari hali inayosababisha vifo vya ghafla.

"Matumizi ya dawa hizo kwa sasa ni makubwa na sisi Mamlaka tumethibitisha kupitia tafiti kuwa mauzo yapo juu na zinatumiwa sana, tena kwa kificho hali ambayo ni hatari kwa kuwa wengi wanazidisha dozi," alisema.

Katika hatua nyengine kwenye mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amewahimiza TMDA kuchukua hatua za haraka, katika kudhibiti matumizi yaliyopita kiasi ya tumbaku.

"Vyombo vya habari vishiriki katika kufanya uchunguzi na kutumia kalamu zao katika kusaidia jamii, kupunguza matumizi hayo ambayo yanachangia ongezeko la magonjwa ya kansa ya koo, ngozi na kifua kikuu,"alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad