Mapya yaibuka ! Mwalimu wa Shule ya Kiislamu Kuhukumiwa Kifo Baada ya Kukutwa na Hatia ya Kuwabaka Wanafunzi 13


Mapya yaibuka ! Mwalimu wa shule ya kiislamu kuhukumiwa kifo baada ya kukutwa na hatia ya kuwabaka wanafunzi 13 na kuwapa mimba wanafunzi 8 😲😲

Mwalimu huyo kwa jina la Herry Wirawan aliwabaka kati ya mwaka 2016 hadi 2021 ambapo mabinti hao walikuwa na miaka kati ya 12 hadi 16, aliwapa mimba wengi wao ambapo wamejifungua na wazazi wao walikuwa hawajui sababu shule ilikuwa ya bweni na ilikuwa mbali na nyumbani. Mabinti hao wengi wametoka familia maskini kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo


Mwaka jana mwanzoni mmoja wa wazazi wa mabinti hao alienda polisi kushitaki baada ya binti yake kurudi nyumbani na kugundua alitoka kujifungua muda si mrefu. Baada ya hapo ndio ikafahamika zaidi kuwa Mwalimu huyo wa shule ya kiislamu amebaka mabinti wengi na walikuwa wanaogopa kuzungumza

Mwezi February mwaka huu baada ya uchunguzi kukamilika mahakama ilimhukumu kifungo cha maisha jela Mwalimu huyo lakini rufaa ikakatwa na sasa hukumu ya kifo ndio inamkabili

Mmoja wa wazazi wa mabinti hao walisema hawakuwa na wasiwasi waliamini kuwa watoto wao wapo sehemu salama lakini kumbe walikuwa wananyanyaswa kingono na Mwalimu wao


Waziri wa haki za watoto nchini humo baada ya uchunguzi alisema hukumu ya kifungo cha maisha jela ilikuwa ndogo anyongwe lakini hata hivyo tume ya haki za binadamu nchini humo inaona kunyongwa sio sawa hiyo ya kufungwa jela maisha ni itamfaa

Mwalimu huyo muda wote mahakamani alikuwa ameinamisha kichwa chake chini

Kesi hiyo ya ubakaji imeibua taharuki kubwa miongoni mwa jamii nchini humo na kushangaa mwalimu huyo kufanya unyanysaji kwa muda mrefu. Wengi wametaka adhabu iwe kali ili iwe fundisho kwa wengine

serikali imeahidi kuwalipa fidia mabinti hao kwa masahibu waliyoyapata kwani baadhi ya walionyanyswa kingono walikutwa na majeraha

Indonesia ndio nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na waislamu wengi zaidi karibia asilimia 87% ya raia wake ni waislamu na ina maelfu ya shule za bweni za kiislamu na shule nyingine za bweni za madhehebu mengine

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad