Marehemu Spika wa Bunge la Uganda Jacob Alipewa Sumu


Nathan Okori ambaye ni Baba mzazi wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Uganda Jacob Oulanyah amesema Mtoto wake (Spika Jacob) alipewa sumu ambayo ndio imesababisha kifo chake.

Mzee Okori ametoa kauli hiyo leo wakati wa shughuli za mazishi ya Spika Jacob.

"Sitaki niomboleze na kulia kwa ndani tu nataka kuweka ukweli wazi, Jacob alipewa sumu, aliniambia kabla hajafariki, sumu ile iliathiri afya yake sana na wakati anasafirishwa kwenda nje ya Nchi (Marekani) kwa matibabu tayari walikuwa wamechelewa na hakuweza kupona"

Jacob alifariki dunia March 20,2022 nchini Marekani alipokuwa akipatiwa matibabu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad