Mashabiki Simba wakataa Yanga isipigiwe kinanda



 
WAKATI Simba na Yanga zinaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza kipindi cha kwanza cha mchezo wa Kariakoo Derby, spika za uwanja wa taifa zilikuwa zilikuwa zinapiga wimbo maalumu wa CAF na suala hilo liliwafanya mashabiki wa Simba uwanja mzima kusimama na kuonyesha ishara ya kukataa.

Mwanaspoti ambayo imekita kambi uwanjani hapa iliwasikia baadhi ya mashabiki wakinyoosha mikono na kuonyesha ishara ya kukataa na wengine wakisema kwamba hawataki.
Wimbo huo maalumu hutumika kwenye mechi zinazohusisha michuano ya CAF ambayo Simba imetolewa wiki chache zilizopita  hatua ya robo fainali dhid ya Orlando Pirates ya Afrika ya Kusini.

Mashabiki wa Simba waliopo ndani ya uwanja  hadi sasa ni wachache na sehemu kubwa ya viti vya upande ambao huka ni tupu.

Kabla ya mchezo huo kuanza beki wa Simba Henock Enonga
aliamsha vaibu la wana Simba kwa kwenda kuwanyooshea mikono na wao wakasimama kumpigia makofi huku wakishangilia.


 
Lakini muda huo huo Mayele naye aliamsha vaibu la wana Yanga kwa kwenda kuwanyooshea mikono kama alivyofanya Enonga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad