Matumizi ya Energy ni BOMU Kwa Vijana Waafrika



"MATUMIZI YA ENERGY NI BOMU KWA VIJANA WAAFRIKA" Ni kawaida VIJANA wa kileo kushindana katika kufakamia Red Bull, Monster Energy, MO Energy na vinginevyo, huku Wengine wakioneshana ubobezi wa kuchanganya Vinywaji Hivyo na Pombe.

Chombo Cha UMOJA wa ULAYA chenye Mamlaka ya kusimamia Usalama wa Chakula(European Food Safety Authority, kimebainisha kuwa Asilimia 30 ya Watu wazima hutumia Energy Drinks, Asilimia 68 Ni Watoto wa Umri wa Miaka 16-18 na Asilimia 18 ni Watoto CHINI ya Miaka 10.                  

Pamoja na Ongezeko la Watoto na VIJANA Wanaotumia, Tafiti zinaonesha kuwa Matumizi ya Vinywaji vya kuchochea nguvu maarufu Kama Energy Drinks, Yana athari Kubwa kwa Afya ya Mwanadamu.                                     

Utafiti uliofanywa na Jopo Wataalam toka Shirika la Afya Ulimwenguni 'WHO,' umethibitisha kuwa vivywaji vya Energy, ambavyo ni mchanganyiko wa kichocheo Cha  Caffeine, sukari, Sodium na Taurine ni  Chanzo kikuu cha MATATIZO ya MOYO, Akili ikiwemo kukosa usingizi, Shinikizo la Juu la DAMU, Shambulio la MOYO, Mpapatiko wa  MOYO(Heart Palpitations), sonona, Kukosa utulivu(Restlessness) na kuishiwa  maji mwilini(dehydration, na vifo vya ghafla, kutokana na Shambulio la MOYO(cardiac arrest).                                                         

Kwa mujibu wa Matokeo ya Utafiti wa Chuo Kikuu cha Toronto ya Mwaka 2015, Matumizi ya Energy Drinks yaweza kupelekea  Athari ya kuharibika kwa UBONGO.Brain Damage.                                                    

Hatari ya Matumizi yya Energy Drinks huongezeka Mara dufu pale vinywaji hivyo vinapochanganywa na Pombe. Kuto          

Athari ya vinywaji Hivyo kwa Watoto zimepelekea Ushirikiano wa Madaktari wa Marekani(American Medical Association) kuzuia Watoto CHINI ya Miaka 18 kutumia Energy Drinks.                           

Dokta Stephen Nguyan MD, Palo Alto wa Taasisi ya Afya wanadai kuwa Matumizi ya vinywaji hivi si SALAMA kabisa. Wakati chupa Moja ya  SODA(COKE, PEPSI) kina  KIWANGO cha Caffeine cha miligramu 35, vinywa vya kuchochea nguvu maarufu Kama Energy Drinks vina Caffeine miligramu kuanzia 150 Hadi 280. Kiwango Cha juu Cha caffeine kwa MTU Mwenye kilo 70 Ni miligramu 210.      

Kuhusu vifo vinavyotokana na Energy Drinks, Dalili  za MWANZO Ni kifua kubana, uchovu, miguu kuvimba, kizunguzungu kikali, kuona giza la ghafla, Kukosa usingizi. Unapohisi Dalili hizo ni king'ora Cha HATARI.                 

Nimeshuhudia VIJANA wawili, wabobevu  wa Matumizi ya Energy Drinks Wakipoteza MAISHA kwa Shambulio la MOYO. VIJANA walioshaurika na kuacha Matumizi ya  vinywaji Hivyo Hadi Sasa wako hai.           

Je, tunapoteza nguvu KAZI kiasi gani kutokana na JINAMIZI HILI? Je, tutakwepaje HATIA ya  kukitoa KAFARA kizazi chetu kwa kigezo feki Cha Kulinda UCHUMI?                 

VIJANA wa  Bara la AFRIKA wapaswa  kulitegua BOMU hili HATARI kwa kwa kupaaza SAUTI Ili Nchi zao ziwe na  SERA  za Kulinda USALAMA WA WATU WAO. Katika hili Tanzania yapaswa kuongoza usukani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad