Mbunge Shabiby atoa Mwarobaini Kupanda bei mafuta



MBUNGE wa Gairo Mohammed Shabib ameitaka Serikali kuruhusu kampuni binafsi kuagiza mafuta wenyewe bila kutumia uagizaji wa pamoja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Shabiby ametoa ushauri huo leo Jumatano tarehe 6 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema mfumo wa uagizaji wa pamoja unafanya kutokuwepo kwa ushindani wa bei na hivyo bei inapopanda kwenye soko ambalo mafuta yanaagizwa kunakuwa hakuna mbadala.

“Leo hii mkiruhusu kampuni binafsi ziagize mafuta na kama mtu anaona kuna unafuu kwenye uagizaji wa pamoja afanye hivyo na kama ataona haina unafuu alete yeye,” amesema.



Ameongeza kuwa zimekuwa zikitolewa hoja za upotoshaji kwamba uagizaji wa mtu mmoja mmoja unasabisha ukwepaji wa ushuru.

“Meli zote zinashusha kwenye mita wanakwepaje ushuru? Hii kazi waachieni TRA utasikia TRA wanakula dili lakini ukiangalia tangu huu mfumo wa uagizaji wa pamoja mita imekufa mara nyingi kuliko kipindi cha uagizaji binafsi,” amesema.

“Naombeni sana turuhusu hayo na bei ya mafuta itashuka kuliko tulivyotarajia na wala tusidanganyane watu kwamba Serikali inaweza kutoa kodi kwenye mafuta, haiwezekani kodi ndiyo inayolipa mishahara na kununua madawa,” amesema Shabiby.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad