‘Mfalme Zumaridi’, Wenzake Wasomewa Maelezo ya Awali



Mwanza. Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Mwanza imewasomea maelezo ya awali katika kesi ya usafirishaji haramu wa binadamu inayomkabili Diana Bundala maarufu ‘Mfale Zumaridi’ na wenzake tisa leo Alhamisi Aprili 28, 2022.

Zumaridi na wafuasi wake wanakabiliwa pia na shtaka la kushambulia na kuzuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao na kufanya kusanyiko lisilo na kibali.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Emmanuel Luvinga amewasomea maelezo hayo ya awali mbele ya Hakimu Mwandamizi, Monica Ndyekobora.

Luvinga ameiambia mahakama hiyo kwamba washtakiwa hao walitenda kosa hilo Februari 23,2022 la kumjeruhi na kumzuia kutekeleza wajibu wake askari polisi, James Mgaya na Afisa Ustawi wa Jamii, Christina Mwisongo nyumbani kwa Mfalme Zumaridi, eneo la Bugugu kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana.


“Vurugu hizo zilipelekea afisa wa polisi na ustawi wa jamii kushindwa kutekeleza majukumu yao, waliondoka eneo la tukio na kuliripoti kituo cha polisi Nyamagana Inspekta Mgaya alipewa PF3 na kupewa matibabu hospitali ya Nyamagana.

“Mnamo Februari 26, askari walifika eneo la tukio kukamata watuhumiwa wote na kuwapeleka kituo cha polisi Nyamagana baada ya kuhojiwa walikiri katika maelezo yao na kufikishwa mahakamani ambapo walifunguliwa shtaka linalowakabili sasa,” amesema Luvinga.

Washtakiwa hao wamekana kutenda makosa hayo, huku Hakimu Ndyekubora kuagiza upande wa Jamhuri kuleta mashahidi.


Kesi hiyo imehairishwa hadi Mei 10, 2022 huku upande wa Jamhuri ikiahidi kupeleka mashahidi 20 na vielelezo vinne

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad