MWANAMKE anayefahamika kwa jina la Rekha ameenda kuililia mahakama ya Rajasthan nchini India akitaka apewe mimba na mume wake anayefahamika kwa jina la Nandlal (34), anayetumikia kifungo cha maisha jela.
Mahakama nchini India baada ya kupitia vifungu vya sheria na imani mbalimbali za kidini ikiwemo Uhindu, Uislamu, na Ukiristo na kuona mojawapo ya mambo muhimu katika maisha ni pamoja na mtu kuendeleza vizazi iliamuru Rekha asikilizwe ombi lake.
Licha ya kwamba mume huyo amefungwa maisha kwa makosa yake Mahakama imetambua kuwa mke wake hana makosa na anastahili kupata haki yake kama mke halali wa mfungwa na kama binadamu ambaye ana haki za msingi za kuendeleza kizazi chake hivyo Mahakama ikaona kuna kila sababu ya kumruhusu mwanaume huyo kwa muda wa siku 15 kwenda kuhudumu kwa mke wake kisha baada ya muda huo arudi Gerezani kuendelea na kifungo chake.
Mfungwa wa kifungo cha maisha akiwa Gerezani
Lakini pia imeelezwa kuwa kwa siku za nyuma mwanaume huyo aliwahi kupewa siku kadhaa za kwenda uraiani na baada ya siku hizo kukamilika mwanaume huyo alirudi mwenyewe kwa hiari yake kitendo ambacho kimeonesha kuwa mfungwa huyo ana nidhamu kubwa na utii wa sheria ndiyo maana Mahakama ikaona kuna sababu ya kumpatia tena ruhusa ya siku hizo 15.