Mgogoro wa Ukraine: Putin kuhutubia viongozi wa Afrika



Rais wa Urusi, Vladimir Putin
RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, anatarajiwa kuhutubia wakuu wa nchi za Afrika, ili kueleza msimamo wake juu ya kinachoendelea kwenye mgogoro wa kivita kati ya nchi yake na Ukraine. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 15 Aprili 2022 na Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Shirikisho la Mambo ya Nje Urusi, Andrey Klimov, katika mkutano wake na waandishi wa habari wa Afrika, uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Klimov amesema, shirikisho hilo litaanda mkutano kati ya Urusi na nchi za Afrika, utakaofanyika Novemba 2022.

“Mwaka huu shirikisho litafanya kazi na Afrika, Urusi itafanya mkutano na Afrika. Mkutano unaokuja utafanyika Novemba 2022. Tutajadili kuhusu hili. Tutafafanua operesheni yetu maalumu ya kijeshi nchini Ukraine, tutarejesha mahusiano yetu ambayo yameharibiwa na nchi za mashariki,” amesema Klimov.


 
Aidha, Klimov amesema, Urusi inaanda mpango maalumu wa kuzisaidia nchi za Afrika, ili kuimarisha mahusiano yao. Huku akiahidi mabalozi wa taifa hilo barani Afrika, watazungumza na maafisa wa masuala ya kigeni wa nchi husika, kuhusu utekelezwaji wa mpango huo.

Amesema kabla ya 2004 Urusi ilikabiliwa na changamoto ya kijamii na kisiasa, baada ya kuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe, lakini ilifanikiwa kuimarisha uchumi wake.

Amesema, kuanzia 2005 hadi 2020, Urusi ilikuwa inarejesha mahusiano yake na nchi za Kisoviet, kama China na India.


“Tutatoa ushirikiano wa kijeshi kwa nchi zote zinazotuunga mkono,” amesema Klimov.

Wakati Urusi ikitangaza kusudio la kufanya mkutano na nchi za Afrika, Rais wa Ukraine, Volodimir Zelensky, ana mpango wa kuhutubia mkutano wa Umoja wa Afrika.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad