Miriam Odemba Afunguka Kuhusu Ibraah "Moyo Wangu Upo Kwa Mtanzania Handsome Boy"


Miriam Odemba(40) afunguka kuhusu Ibraah(23)

"My love, kila binadamu aliyeumbwa na hisia huwa ana sehemu ya kuupumzisha moyo wake, kiukweli mimi mwili wangu unaishi Paris, Ufaransa lakini moyo wangu naupumzisha Tanzania, tena nisifiche hisia zangu ni kwa Mtanzania asie na shida na mtu, ni kijana, handsome boy, mkarimu, mpole , mpambanaji na anayejali

Hayo mengine ya hivi mara vile ni ya wananzengo, kwa hiyo nakushauri wewe msichana, wewe mwanamke na wewe mwanaume usije ukaficha hisia zako kwa kuwaogopa wajumbe wa Instagram, jali hisia zako." Ameandika Miriam Odemba mwanamitindo wa kimataifa anayeishi Paris, Ufaransa

Mrembo huyo ambaye aliwahi kushika nafasi ya 2 katika shindano la dunia la Miss Earth 2008 nchini Ufilipino hata hivyo bado amewaweka njia panda mashabiki kwani alishasema pia yeye na Ibraah ni 'marafiki tu'

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad