Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Wilbrod Mutafungwa amepiga marufuku Dereva au Kondakta kushuka na kumfuata Trafiki nyuma ya gari pindi wanaposimamishwa barabarani
Amesema "Jeshi ni Taasisi kubwa, wapo (Trafiki) wachache inatokea wanajihusisha na vitendo vya rushwa, hivyo huwezi kusema Jeshi zima linahusika na rushwa. Taratibu zipo za kuwachukuliwa hatua na huwa inafanyika hiyo"
Mutafungwa amesema hayo baada ya kuwepo malalamiko ya rushwa dhidi ya Askari wa Usalama Barabarani (Trafiki) wanaosimamisha magari hasa daladala na Madereva au Makondakta kuwafuata na ‘kumalizana’ nao nyuma ya gari
#JamiiForums