Kijuu juu wengine wataona ni pesa kubwa ila jamaa anastahili zaidi ya hiyo per post. Amejibrand mwenyewe halafu mashabiki wake wengi ni wa nje baada ya wengi huku kumpuuza mwanzo kwahiyo lazima aweke standard flani.
Kingine Kibongo bongo wengi wana wachukulia content creators kama watu waliopo kwa ajili ya kupoteza muda wakati imegeuka kuwa serious career kwa watu ambao mwanzo walionekana kama haziwatoshi hivi au hawana kazi ya kufanya
Mfano mzuri ni Khabby, by 2019 alikuwa hana kazi baada ya corona kutetemesha uchumi wa dunia, maisha yake alikuwa haijui kesho yake vizuri. Lakini akaona fursa ya mitandao ya kijamii kitu kama utani tu kwasasa maisha yake yamegeuka kuwa ndoto ya mafanikio hata kwa waliomcheka.
Kwasasa Khabby amekuwa milionea $$$$ ndani ya miaka miwili tu na Kibongo bongo Khabby sio milionea ila ni bilionea katika umri mdogo tu
Kili Paul anastahili zaidi ya hiyo milioni 7 kwa post moja na sio laki moja sijui laki 5. Halafu target yake Ni kupata pesa nje sio Bongo labda kampuni kubwa za Bongo