Morrison Aonywa Kuhusu VAR Uwanja wa Mkapa, Dar Leo Dhidi ya Orlando Pirates



KUFUATIA kutumika kwa mara ya kwanza mfumo wa video wa kumsaidia mwamuzi (VAR) hapa Tanzania katika mchezo wao wa leo Jumapili dhidi ya Orlando Pirates, Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco amewaonya mastaa wake akiwemo Bernard Morrison kuhakikisha hawafanyi makosa ya kumtegea mwamuzi.

Simba leo Jumapili majira ya saa 1:00 usiku, watashuka Uwanja wa Mkapa, Dar, kuvaana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza na Spoti Xtra, kuhusu matumizi ya VAR, Kocha Pablo alisema: “Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo huu dhidi ya Orlando.

“Kuhusu uwepo wa VAR, kwanza naweza kusema ni mfumo bora ikiwa unaweza kutumiwa, kwangu hili si jambo jipya, nimewahi kusimamia michezo VAR ikiwepo, hivyo naijua vizuri.

“Kwa wachezaji wangu nadhani wengi wao hii itakuwa mara ya kwanza kuitumia, tumelifanyia mazoezi hilo na nimewaambia sababu pekee ya kusimamisha mpira ni mpaka refa aamue hivyo.

“Kwenye uwepo wa VAR hatupaswi kutegea uamuzi wa refa peke yake kwani unaweza ukadhani ni mpira wa kuotea kumbe sio, najua kutakuwa na makosa kidogo lakini lazima tuhakikishe tunafanya vema.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad