UONGOZI wa Orlando Pirates, umewataja wachezaji kama Bernard Morrison na Pape Ousmane Sakho kuwa ni wachezaji wa kuchungwa katika mchezo wao kutokana na ubora wao waliouonyesha katika mchezo uliopita ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya USGN ya nchini Niger.
Orlando Pirates ambao wamepangwa kucheza na Simba katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, wataanzia ugenini katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Aprili 17.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Orlando, Floyd Mbele, alisema kuwa ametazama baadhi ya mechi za Simba katika michuano hiyo huku akiwaona wachezaji kama Sakho na Morrison kuwa na mchango mkubwa ndani ya timu hiyo, watu ambao ni wa kuchungwa kuelekea katika mechi yao.
“Tuna mchezo mgumu sana mbele yetu kutokana na ubora wa wachezaji wa Simba, nimetazama baadhi ya michezo yao nimewaona wachezaji wengi wazuri kama Bernard Morrison na Sakho, ni wachezaji wazuri.