Mpenzi Mpya wa Diamond Anapenda Magauni Mekundu, Jina Lake Hili Hapa



Mtaalam Fundi Manyumba ambaye pia anajiongeza kama mwanamuziki na mtangazaji katika kituo cha bosi wake cha Wasafi, Babalevo anaendelea kuwachezesha mashabiki vwa msanii Diamond karata tata na kali kwa kulifichua jina la mpenzi wake ambaye kulingana na mamake Diamond, Mama Dangote, ni bibi harusi mtarajiwa.

Baba Levo alianza harakati za kuliweka wazi jina la mpenzi wa msanii huyo kwanza kwa kuwataka mashabiki kumwaga maoni zaidi ya elfu mbili na mia tano ambapo alifichua herufi moja tu ya jina hilo ambalo alisema herufi A imo katika jina la ‘mke’ mpya wa Diamond.


Msanii huyo hatimaye amefanya kufuru ya karne baada ya kufichua zaidi kwamba jina lenyewe halina herufi U ila akazidi kubainisha kwamba herufi R ni miongoni mwa herufi zinazolitunga jina hilo.

“Mke wa Diamond jina lake halina herufi U, ila herufi R ipo,” aliandika Baba Levo kwenye Instagram yake.

Kwa kuchora taswira kamili vichwani mwa mashabiki, Baba Levo alizidi kumwaga mtama kwamba mwanamke huyo ambaye ni bibi harusi mtarajiwa anapenda sana kuvalia magauni ya rangi nyekundu


Kwa mara nyingine tena kama tulivyodadisi hapo awali, Zuchu ambaye wengi wamekuwa wakimsema kuwa ndiye mpenzi wa Diamond anaonekana kutupiliwa nje na mbali kabisa kutokana na vidokezo ambavyo Baba Levo anazidi kuviachia.

Juzi aliposema kwamba mpenzi mpya wa Diamond jina lake halina herufi A, hilo moja kwa moja liliondoa Zuchu katika orodha hiyo, na hivi sasa Levo anavyosema hamna cha herufi U, herufi ambayo inaonekana mara mbili kwa jina la Zuchu, basi mashemeji itabidi mmekubali Zuchu hayupo kwenye listi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad