Kampuni ya picha za satelaiti Maxar Technologies imetoa picha za kile inachosema ni msafara mkubwa wa kijeshi wa Urusi, ulioko mashariki mwa Kharkiv.
Picha hizo, zilizopigwa tarehe 8 Aprili, zinaonyesha mamia ya lori za magari ya kivita yenye mizinga ya kukokotwa, na magari mengine ya kijeshi - yakienda kwa karibi maili nane (12km) na kuelekea kusini kupitia mji wa Velykyi Burluk wa Ukraine.
Katika ujumbe wa Twitter, mchambuzi wa masuala ya kijeshi George Barrow - akiwa na Taasisi ya Utafiti wa Vita (ISW) - alisema kuwa kuna uwezekano msafara huo ulikuwa unaelekea kusini katika mji wa Izyum. BBC haijaweza kuthibitisha dai hili kwa uhuru.
Vikosi vya Urusi viliuteka mji wa Izyum wiki iliyopita na wamekuwa wakiutumia kama uwanja wa kuelekea Sloyansk, mji ambao ni muhimu kwa lengo la Moscow la kuteka eneo lote la mashariki mwa Ukraine.
Vikosi vya Urusi hivi karibuni vimeuteka mji wa kimkakati wa Izyum na kuutumia kama kituo cha kushambulia Sloyansk, kusini mwa nchi hiyo.
ISW inasema ikiwa Ukraine itashikilia Sloyansk, kampeni ya Urusi ya kuteka maeneo ya mashariki ya Donetsk na Luhansk "itafeli