MSEMAJI wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari na ameahidi kuitumikia vema kampuni hiyo katika kuhakikisha inafikia malengo yake,
Kampuni ya Moovn ni kampuni maalum kwa ajili ya biashara ya usafirishaji wa abiria na lengo kuu ni kuwasaidia watanzania katika kutatua changamoto ya usafiri lakini pia kutoa fursa ya biashara kwa madereva na vijana wa kitanzania.
Akiongea na waandishi wa habari meneja masoko wa kampuni hiyo Jafar Wazir Kassim amesema kuwa mwekezaji wa Kampuni hiyo ni Mtanzania ambaye anaishi Marekani kwahiyo kampuni hiyo ni kampuni ya mzawa wa Tanzania.
Balozi wa Moovin Tanzania akisaini Mkataba wa kazi
Meneja huyo amesema Kampuni yake imekuja kitofauti ikiwa imeshafanya tafiti na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo malipo kwa madereva pamoja na usalama wa mazingira ya kazi kwa dereva na abiria wake lakini pia manufaa endelevu ya dereva.
Katika kutibitisha hilo Jafar Waziri amesema kuwa Kampuni ya Moovin Tanzania imekuja na mfumo utakaomruhusu dereva kuchukua kiasi chake cha pesa kama malipo papo kwa papo mara baada ya kumaliza safari yake.
Manara amewaomba watanzania kuiunga mkono kampuni ya Moovin kwani ni kampuni ya muwekezaji mzawa.
Kwa upande wake Balozi wa Kampuni hiyo Haji Sunday Manara amesema anaahidi kufanya kazi bega kwa bega lakini pia akiomba kuungwa mkono kutoka kwa watanzania wote kuhakikisha kampuni hiyo inafikia malengo.
Manara ameendelea kusisistiza kuwa muwekezaji ni mtanzania kwahiyo kuna kila haja ya kumuunga mkno muwekezaji mzawa ili aweze kufanya kazi ambayo kimsingi itawasaidia hata watanzania wengine katika kupunguza ukali wa ugumu wa maisha hasa kwa madereva watakaopata fursa ya kufanya kazi na Kampuni hiyo.