Msemaji wa Yanga SC, Haji Manara ametia neno kwa Klabu ya Simba SC kutoka Tanzania kukutana na Orlando Pirates katika kombe la shirikisho barani Afrika. Manara alitia neno kupitia uwanja wa maoni kwenye post ya Instagram ya Orlando Pirates ya ratiba ya klabu hiyo kukutana na Simba SC kwenye michuano hiyo.
"Wananchi wenzenu mtatukuta huku huku,,Njoooni Wanaume @orlandopirates Vivaaaaaaa" Aliandika Haji Manara. Ratiba hii ya Wekundu wa Msimbaji kukutana na klabu hiyo ya Afrika Kusini ilipangika baada ya droo ya Robo Fainali ya Michuano hiyo iliyochezeshwa leo April 04.