Well ni msimu ambao inaonekana wazi Yanga ana uwezekano mkubwa wa kutwaa ubingwa baada ya misimu minne, baada ya muda mrefu wa kujaribu na kufeli ni sasa kama hesabu zao zinaenda sahihi
Kwa mechi zilizosalia na utofauti wa alama basi uwezekano ni mkubwa kwa Jangwani labda maajabu ya mpira wa miguu yatokee, timu haijapoteza mchezo mpaka sasa, inakosa baadhi ya wachezaji ila bado iko imara
Katika hatua ya kwanza nasema Yanga ni bingwa apewe taji lake msimu huu, utofauti wa alama ni mkubwa, tayari timu vigogo kama Azam wameachia alama, timu pekee iliyosalia ni Simba ila nyingi Yanga anapewa nafasi akicheza nazo
Lakini kwanini Simba nae apewe ubingwa msimu huu?? Apewe ubingwa upi??
To me naona wanastahili ubingwa kwa heshima kubwa ya TRANSITION wanayofanya kwenye mipango mikakati ya klabu yao, kuna kitu ambacho wengine wote wanastahili kukiiga kutoka kwao
Wapo nafasi ya pili kwenye ligi nyuma ya Yanga ila hawana presha kubwa wanaendelea kucheza mechi zao huku wakipiga hesabu zao kwa usahihi, wapo kwenye FA, wapo Ligi kuu bara na wapo Shirikisho Afrika, kote wapo hatua nzuri
Inakupa tafsiri kubwa juu ya Management yao, sio rahisi kuwa na malengo matatu na yote yakaendana, yote ukawa kwenye hatua kubwa, huwa tunaona kuna baadhi ya timu huamua kupigania kikombe kimoja na kuipa nguvu yote
Huenda Simba wanaweza wasitwae kikombe cha Ligi kuu ila wanatwaa ubingwa wa darasa la bure kwa klabu nyingi, bado kupitia ushiriki wao kimataifa umesaidia kupeleka timu nne kwa mara ya pili mfululizo
Nafasi nne zilizopatikana zinaongeza chachu kwenye ligi, kwenye vita ya kupata hizo timu! Bado inaongeza thamani ya ligi, inatangaza nchi kimataifa, nje ya ubingwa wa Yanga pia kuna ubingwa wa Simba
Anapopewa taji Yanga msimu huu, kuna taji ambalo pia Simba analibeba tena na tena kwa heshima ya mpira wa miguu, IKITOKEA