Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili kutoka Nigeria aitwaye Sis Osinachi Nwachukwu maarufu kwa wimbo wake "Ekwueme" amefariki dunia.
Osinachi alifariki dunia jioni (April 8, 2022) hii baada ya kupambana na ugonjwa usiojulikana kwa takriban miezi miwili huku vyanzo vingine vikidai ni kansa ya koo.
Baadhi yake nyimbo ni pamoja na "Nara Ekele" akiwa na Mchungaji Paul Enenche (Dunamis,Abuja), "Ekwueme" akiwa na Prospa Ochimana na nyinginezo.
Wimbo wa Ekwueme umejipatia umaarufu sana kutokana maudhui yake huku ukitasambaa na kuimbwa na jamii kubwa duniani.
RIP.