Mume wa Shilole "Tumepitia magumu katika Ndoa hii na Shilole"



Mwanamuziki na mjasiriamali maarufu nchini Shilole, leo Aprili 20, 2022 ni siku anayotimiza mwaka mmoja tangu alipofunga ndoa na mumewe Rommy3D.


Wawili hao kwa pamoja wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kutumiana jumbe za upendo kama sehemu ya kusherehekea mwaka mmoja wa ndoa yao.

Shilole ameenda mbali zaidi na kudokeza kuhusu historia fupi ya penzi lao, wakati waliokutana, kuachana na kurudiana tena mapaka hatma ya kufikia uamuzi wa kuwa wanandoa.


“Nilimfahamu Rajabu miaka mingi kidogo iliyopita. Maisha yana siri zake na mapito yake, tukapita pamoja tukatengana halafu kudra za Mungu zikaturudisha pamoja tena kama miaka miwili iliyopita.


Mungu ndiye muandishi wa hadithi za maisha yetu, yeye mwenyewe anajua kwa nini tulitengana na kwanini nilipitia yote niliyopitia kabla ya kukutana tena na mume wangu.

Ninachojua mimi, kukutana tena na Rommy na kufunga naye ndoa ni zawadi kubwa zaidi niliyokirimiwa na Allah.

Ndoa hii ndio nilichotaka, Mume huyu ndiye niliyestahili, hata wakati ule ‘mnabet’ kuwa ndoa itadumu mwezi mmoja na mimi nilimuachia Mungu aamue hatma yetu kwa rekhma zake.

Tuko hapa kwa uwezo wa Mungu na yeye Inshaalah ataendelea kulinda ndoa yetu.

Tunamshukuru Mungu leo tunapotimiza mwaka mmoja wa ndoa yetu. Namshukuru Mume wangu kwa kuendelea kuwa mume bora kwangu na kiungo muhimu cha furaha kwetu. nakupenda sana Mume wangu,” ameandika Shilole.

Kwa upande wa mume wa Shilole Rommy 3D yeye ameweka wazi mambo kadhaa kuhusu magumu waliyoyapitia na namna walivyojikita katika kutimiza lengo la wao kuingia kwenye ndoa bila kusikiliza maneno ya watu ambao kundi kubwa lilikuwa likitabiri kuwa pengine wawili hao hawatafika popote.

“Siku ya leo tunasherehekea mwaka mmoja wa ndoa yetu najua kinaweza kua ni kipindi kifupi ukilinganisha na watu wengine ambao wamekaa miaka mingi zaidi ndani ya ndoa zao lakini kwa upande wangu siku 360 ni nyingi sana kuweza kusherehekea katika ndoa yangu kwa sababu sio rahisi kama inavyoonekana hasa ukizingatia mke wangu ni mtu maarufu ambae anapendwa karibuni na kila mtu (Alhamdulillah).

Kukatishwa tamaa, kudharaulika, kupingwa kutabiriwa mabaya ndio imekua style ya maisha yetu lakini Mungu ni mkubwa kuliko chochote still tuko pamoja na Inshallah tuna miaka mingi mingine inakuja kwa kua Mungu anatupigania, mke wangu Shilole nakupenda sana,” ameandika Rommy kupitia ukurasa wake wa mtandao wa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad