Viongozi Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamezindua ramani mpya ya Jumuiya hiyo ambayo inamjumuisha mwanachama mpya wa Jumuiya hiyo (DRC).
Uzinduzi huo umefanyika baada ya Rais wa DRC Mhe. Felix Tshesikedi kusaini makubaliano ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
DRC ilijiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Machi 29, 2022 na kuwa mojawapo ya nchi Saba zinazounda Jumuiya hiyo.