Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majangili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Katavi kwa tuhuma za kukutwa na silaha mbalimbali ndani ya hifadhi ya Taifa ya Katavi, Baadhi ya silaha walizokutwa nazo ni Gobore, gololi za chuma, shoka, visu na pembe moja inayodhaniwa kuwa ni ya Swala
Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi Ali Hamad Makame amesema watuhumiwa hao ni wakazi wa Mkoani Rukwa.
Aidha Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa kumi wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo uvunjaji nyumba na kuiba thamani za ndani,uporaji wa simu na pochi za wanawake.
Katika tukio nyingine mtoto Cosmas Abdala Amani (13) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita amepoteza maisha baada ya kuzama kwenye maji wakati anaogelea na wenzake wawili kwenye mto Kasimba.