Mwanaume mmoja katika Wilaya ya Kagadi, Magharibi mwa Uganda ameingia kwenye rekodi ya aina yake baada ya kupambana vikali na simba dume na kufanikiwa kumuua huku naye akijeruhiwa vibaya.
Baada ya kumuua simba huyo, maafisa wa mamlaka ya wanyama pori walifika eneo la tukio kuthibitisha tukio hilo huku majeruhi akikimbizwa hospitali.