Mwanaume mmoja anaefahamika kwa Jina la Shabani Maulana,(47) Mkazi wa kijiji cha Juhudi A kata ya Chinongwe wilayani Ruangwa mkoani Lindi, amefanikiwa kuua Fisi wawili kwa panga ambao alipambana nao wakiwa wameingia katika zizi la mbuzi lililopo nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa mashuhuda wanasema tukio hilo lilitokea majira ya Saa Kumi usiku tarehe 5/4/2022 ambapo waliingia zizini Fisi 3 kwa lengo la kushambulia Mbuzi waliopo, ndipo jamaa huyo alipowashtukia na kuingia zizini akiwa na upanga huku akiwaomba majirani wamfungie mlango kwa nje ili apambane nao Fisi hao.
Baada ya muda Bwana Shabani alifanikiwa kuua Fisi 2 kati ya 3 walioingia zizimi humo huku 1 akitajwa kukimbia na katika kurupushani hizo Shabani alipata majeraha sehemu ya paja ambapo inaelezwa alikimbizwa kituo cha afya Chinongwe na kupatiwa matibu huku ikielezwa kuwa hali yake kwa sasa inaendelea vizuri.
#CloudsDigitalUpdates