Mwandaaji wa Miss Rwanda Matatani Kwa Kuwadhalilisha Kingono Washiriki




Jeshi la Polisi nchini Rwanda linamshikilia mwandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Rwanda, Dieudonné Ishimwe kwa tuhuma za kuwadhalilisha kingono washiriki wa shindano hilo.

Mpelelezi mkuu wa Serikali nchini humo amethibitisha kukamatwa kwa Mwandaaji huyo, ambapo amesema iwapo atakutwa na hatia adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 15 jela.

Kukamatwa kwa Dieudonné Ishimwe, ambaye ni mtendaji mkuu wa Rwanda Inspiration Back Up, kampuni inayoandaa shindano hilo, kunakuja mwezi mmoja tu baada ya shindano la mwaka huu.

Miss Rwanda ni moja ya matukio yanayofuatiliwa zaidi nchini Rwanda, mfanyakazi mmoja wa kampuni inayoandaa shindano hilo amezungumza na BBC na kuiambia kuwa, wasichana wanne waliogombea mwaka jana na mwaka huu walitoa malalamiko kwa wachunguzi kabla ya kukamatwa kwake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad