Mpiga picha na mtengeneza makala za video wa Ukraine, Maks Levin aliyekuwa na umri wa miaka 40 amekutwa amekufa karibu na mji mkuu wa Kyiv baada ya kutoweka zaidi ya majuma mawili yaliyopita.
Kupitia ukurasa wake wa telegram msaidizi wa rais wa taifa hilo, Andriy Yermak amesema marehemu ambae alipotea tangu Machi 13, mwili wake ulipatikana jana Aprili Mosi karibu na kijiji cha Guta Mezhygirska.
Asasi moja ya kiraia, iiliyonukuu uchunguzi wa awali kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka ilisema mwandishi huyo aliuliwa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wawili wa Urusi.
Itakumbukwa mwandishi huyo katika kipindi cha mapigano kati ya wanajeshi wa Ukraine na Urusi yenye kuungwa mkono ya mwaka 2014, alifanikiwa kutoroka katika mji ambao mamia ya wanajeshi wa Ukraine waliuwawa