Mwimbaji The Weeknd ambaye ametajwa kuchukua nafasi ya Kanye West kwenye tamasha la Coachella, amehitaji kulipwa (USD 8M) zaidi ya TSh. Bilioni 18, kiasi cha pesa ambacho Kanye West alikuwa alipwe kwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo.
Siku chache zilizopita YE aliripotiwa kujiondoa kwenye orodha ya watumbuizaji kinara wa tamasha la Coachella pamoja na Travis Scott. Jana The Weeknd pamoja na kundi la Swedish House Mafia walitajwa kuchukua nafasi hiyo.