Mwimbaji nyota wa bongofleva msanii @officialnandy amempa zawadi ya ndege Kasuku mpenzi wake @billnass, akibainisha kuwa ni ishara ya upendo na kumtaka mpenzi wake huyo awatunze kwa moyo wake wote kama anavyotunza penzi lao.
Aidha Nandy ameeleza, amewachukua Kasuku hao wadogo kwa lengo la penzi lao kukua nao mpaka mwisho wa maisha yao.
Wanandoa hao watarajiwa, majina yao halisi waliyopewa na wazazi wao ni Faustina Charles na William Lymo.