Ndege hiyo ya majaribio ilikamilisha safari ya saa tatu kutoka Uwanja wa Ndege wa Blagnac huko Toulouse hadi makao makuu ya Airbus ya Ufaransa mnamo Machi 25.
Ndege hiyo Iliendeshwa na mafuta aina ya Sustainable Aviation Fuel au SAF ambayo mara nyingi hutengenezwa kwa mafuta ya kupikia yaliyotumika na takataka na inafanya kazi kwa injini moja ya Rolls-Royce Trent 900.
Mafuta yaliyotumika yalitolewa na TotalEnergies, kampuni iliyoko katika eneo la Normandy nchini Ufaransa.
Airbus imekuwa ikifanya majaribio ya matumizi ya safari za ndege zinazotumia SAF kwa kipindi cha mwaka mmoja, huku A350 ikijaribiwa Machi 2021, na ndege ya njia moja ya A319neo ikiruka kutumia mafuta ya kupikia mnamo Oktoba.
Kampuni hiyo inatarajia kupata kibali cha ndege yake kuruka kwenye SAF ifikapo mwishoni mwa muongo huu.
Hivi sasa, ndege za Airbus zinaweza kuendeshwa na hadi 50% ya SAF, iliyochanganywa na mafuta ya taa ya asili.
Airbus inapanga kuzindua ndege ya kwanza duniani isiyotoa hewa chafu sokoni ifikapo mwaka 2035.