Bandari ya Dar es Salaam imeweka rekodi ya kupokea meli kubwa yenye urefu wa mita 189.45 ikiwa na shehena ya magari 4,041 ikitoka Japan.
Kati ya magari hayo 2,936 yanakwenda nje ya nchi, Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Eric Hamissi amesema hayo ni matunda ya maboresho waliyofanya.