Polisi "Kesi ya Raia wa Nigeria Zainab Ilikosa Mashiko ya Ushahidi Alidai Anamtambua Mtuhumiwa Kwa Harufu"




Kamanda wa Polisi Mkoa wa kaskazini Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi Martin Leo Otieno amesema kesi iliyoripotiwa na Raia Mmoja wa Nigeria alifahamika kwa jina la Zainab Oladehinde Ilikosa mashiko ya kufikishwa mahakamani kwasababu ya Kukosekana Ushahidi madhubuti

Kamanda Martin amesema kesi hiyo ya kudhalilishwa ambayo iliripotiwa April 18, 2021 na Raia mmoja wa Nigeria ambae alikua Zanzibar kwa mapumziko ya kawaida huko katika hotel ya Warere iliyopo Nungwi ndani ya Mkoa huo na kudai kuwa alidhalilishwa na mmoja ya mvulana ambae aliingia chumbani kwake alipokua katika hotel hiyo

Kamanda Martin Amesema kesi hiyo baada ya kufanyiwa upepelezi jarada lilifikishwa ofisi ya DPP na kushindwa kufikishwa mahakamani baada ya ofisi ya DPP kutoridhishwa na ushahidi uliotolewa ambapo Raia huyo wa Nigeria alisema anamtambua mtuhumiwa kwa harufu

Hii inakuja siku chache baada ya Raia huyo wa kigeni wa Nigeria kusambaa taarifa ya kufanyika kwa tukio hilo ambalo kwa mujibu wa taarifa tukio hilo limefanyika Mwaka jana

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad