Putin Tajiri Namba Moja Duniani, Anayeitikisa Marekani







WAKATI mtandao maarufu duniani wa Forbes ukimuorodhesha Mhandisi na Mjasiriamali Elon Reeve Musk kuwa na tajiri namba moja duniani kwa kuwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 229 (sawa na Tsh trilioni 530), Rais wa Urusi, Vladimir Putin anadaiwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 263 sawa na Sh trilioni 610.

Hayo yanajiri wakati mmoja wa mabinti zake akitajwa kuwa na utajiri wa bilioni 231 kwa mujibu wa mtandao wa Maily Online.

Putin ambaye ameamuru majeshi yake kuivamia Ukraine tangu tarehe 24 Februari mwaka huu, tayari anadaiwa kumtia nyuma ya nondo mpinzani wake mkuu, Alexei Navalny.

Alexei Anatolievich Navalny ambaye ni mwanasiasa wa Urusi na mwanaharakati wa kupambana na ufisadi, ndiye aliyeanza kufichua utajiri huo wa Rais Putin kiasi cha kuitetemesha Ikulu ya Kremlin.


Kabla ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 13 Februari mwaka jana, Navalny kwa kushirikiana na timu yake alifichua jinsi Putin anavyotumia mtandao wake kupitia watoto, ndugu na washirika wake wa karibu jeshini (KGB), kuchota mabilioni ya nchi hiyo tajiri duniani.

Kwa mujibu wa Maily Online, Navalny ambaye awali alikuwa Meya wa mji wa St Petersburg, alieleza kuwa mmoja wa marafiki wa Putin tangu utoto ana utajiri wa Dola za Marekani milioni 500.

Pia mpwa wake ambaye ni bosi wa kampuni ya mafuta nchini humo anatajwa kuwa na utajiri wa dola za Marekani milioni 500 vilevile.


Aidha, imeelezwa kuwa Shirika la Kitaifa la Uhalifu nchini humo linalojiita ‘kikosi cha kleptocracy’ lilianzisha msako wa mali za Putin nchini Uingereza ambapo wanaharakati walifichua kuwa mmoja wa mabinti zake ambaye alimzaa na mmoja wa wasaidizi wake wa ndani, ana utajiri wa dola za Marekani milioni 100.

Kinachojulikana zaidi hasa baada ya vielelezo kusambazwa mitandaoni ni kwamba Putin anamiliki jumba kubwa la kifahari kwenye ufuo wa Bahari Nyeusi lenye thamani ya dola za Marekani bilioni moja likiwa na vyoo na mabafu yenye thamani ya dola bilioni 650.


Aidha, kwa mujibu wa mwanasiasa huyo wa upinzani – Navalny inaelezwa kuwa jumba hilo lilijengwa kwa ufadhili wa washirika wa Putin waliopata dili za mafuta na gesi nchini humo.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa Putin ana utajiri uliofichwa katika sehemu mbalimbali duniani kwa njia ya fedha, biashara na uwekezaji unaosimamiwa na washirika wake wa karibu.


PUTIN ANASEMAJE?

Itakumbukwa kuwa siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018 nchini humo, Rais Putin alianika kiasi cha fedha alizojipatia kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia 2018 ambacho si kikubwa kama ambavyo ilifikiriwa.

Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Urusi wakati huo ilieleza kuwa, Rais Putin alijipatia mapato ya Rouble milioni 38.5 za Urusi sawa na zaidi ya Tsh bilioni 1.9 kati ya mwaka 2011 na 2016.

Hata hivyo, Putin mwenyewe alisisitiza kuwa anapokea mshahara wa Dola za Kimarekani 92,245 kwa mwaka.

Lakini kwa mujibu wa Gazeti la Washington Post, Rais Putin pia aliorodhesha akaunti 13 za benki mbalimbali ambazo kwa pamoja zilikuwa na akiba ya Dola za Kimarekani 307,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 650.


Rais Putin pia aliorodhesha kumiliki nyumba zake mjini St Petersburg, hisa katika benki moja pamoja na magari mawili ya kimichezo ya nyakati za uliokuwa Muungano wa Kisovieti wa Urusi (USSR).

PUTIN NI NANI?

Rais Putin aliyezaliwa Oktoba 7, 1952 ni Mwenyekiti wa Chama cha Kisiasa cha Muungano wa Urusi na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa nchi hiyo wa Belarus.

Alikaimu kiti cha urais mnamo Desemba 31, 1999 mara baada ya Rais Boris Yeltsin kujiuzulu ghafla, na kisha Putin akashinda uchaguzi wa rais mwaka 2000.

Mwaka 2004, alichaguliwa upya na kushinda, hivyo kuendelea na kipindi chake cha pili hadi Mei 7, 2008 kabla ya kuachia utawala wa nchi kwa Damitry Medvedev aliyeshinda kiti cha urais.


Medvedev kwa kutambua umuhimu wa Putin, mara moja alimteua kuwa Waziri Mkuu katika kile kilichoelezwa kuongoza kwa pamoja bila kinyongo (tandemocracy).


Jina lake lina asili ya watu wa mashariki mwa Urusi likiwa na maana ya mila katika mji wa Leningrad alikozaliwa.

NI LUTENI KANALI

Kwa miaka 16 Putin alikuwa Ofisa Mwandamizi wa Jeshi la Urusi likifahamika kwa kifupi KGB, akipanda cheo hadi kufikia Luteni Kanali kabla ya kujiuzulu na kuingia kwenye siasa akijiunga na chama kilichoanzishwa huko Saint Petersburg, mwaka 1991.

Baada ya kuwa kwenye chama hicho kwa miaka mitano, mwaka 1996 alihamia jijini Moscow kuungana na utawala wa Rais Boris Yeltsin ambako alipaa kwa haraka hadi kuteuliwa kuwa kaimu rais Desemba 31, 1999 baada ya Yeltsin kujiuzulu ghafla.

Septemba 2011, Urusi ilifanya Marekebisho ya Katiba yake katika kipengele cha muda wa rais kukaa madarakani. Marekebisho ya kutoka miaka minne hadi sita na Putin akatangaza kuwania madaraka ya urais kwa mara ya tatu katika uchaguzi uliofanyika Machi 2012.

Nia hiyo ya Putin ilipingwa kwa maandamano katika miji mbalimbali nchini Urusi, lakini alipambana na kushinda.


Mipango mingi ya Putin haipiti kwa wepesi kwani huwa inakutana na changamoto au vikwazo vingi kutoka kwa watu wa kawaida hadi hata waangalizi wa kimataifa kuona kuwa demokrasia imekiukwa, lakini mwisho wa siku, anashinda.

Tangu mwaka 2011, Putin amekuwa mbabe akitangaza Urusi yenye mabadiliko ya kweli katika kila sekta badala ya kuwa na serikali isiyo na mamlaka.

AMETALIKIWA

Rais Putin mwenye umri wa miaka 68, ana watoto watatu wa kike, wawili kati yao wamezaliwa ndani ya ndoa na mmoja nje ya ndoa baada ya kuchepuka msaidizi wa ndani alipoingia Ikulu mwaka 2000.

Aidha, mwaka 2013 Putin alitalikiana na mkewe wa ndoa Lyudmila Putina baada ya kudaiwa kuchepuka tena na mwanadada Alina Kabaeva.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad