Raia Nchini Kenya Ahukumiwa Kifo Baada ya Kuiba Gari la Rais Kenyatta



Kijana aliiba gari la Kenyatta kwenye msafara wake
MWANAUME mmoja raia wa nchini Kenya ambaye anadaiwa kuiba gari la Rais Uhuru Kenyata mwaka 2014 amehukumiwa kifo.

Mwanaume huyo anadaiwa kuiba gari aina ya BMW 735 ambalo lilikuwa na thamani ya dola za kimarekani 10200 kwa wakati huo na lilikuwa katika msafara wa rais na hiyo ni kwa mujibu wa vituo vya habari vya taifa la Kenya ambavyo viliripoti taarifa hiyo kwa mwaka huo.

Wakati akitoa hukumu hiyo hakimu mfawidhi wa mahakama ya Mlimani francis amesema mtu huyo ambaye ni mtaalamu au fundi wa umeme amepewa adhabu hiyo kali kwa sababu ya vitendo vyake kuhusiana na usalama wa taifa.

Mwanaume huyo akiwa na wanaume wengine wawili walimpora inspecta mkuu wa polisi David Machui kwa mtutu wa bunduki tarehe Augost 26, 2014 katika Jiji la Nairobi Nchini Kenya.


 
Inaelezwa kuwa watu hao walikuwa na bunduki aina ya Ak 47 na bastola nyingine wakati wa kutekeleza uhalifu huo, na huo ni kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani.

Watu hao wakaripotiwa kumvua nguo inspector huyo wa polisi na kumtelekeza katika kichaka.


Amehukumiwa kunyongwa mpaka kufa
Inaelezwa kuwa bwana huyo mara baada ya kuwa wamefanikisha jambo hilo alikwenda katika gereji moja iliyopo katika jiji la nairobi na kisha kuondoa mfumo uliokuwa ukifanya gari hilo kufatiliwa na kuondoka zake katika taifa la uganda.


Inaelezwa kuwa polisi wa kenya kwa kushirikiana na polisi wa uganda walianza msako kwa kumtumia mpenzi wake ambaye alikubali na kuanza kutengeneza miadi ya kukutana iliyofanikisha kukamatwa kwake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad