Rais Samia amteua Sophia Simba


Rais Samia amteua Sophia Simba
mwananclm. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT), Sophia Simba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Ustawi wa Jami (ISW).

Tarifa iliyotolewa leo Jumatano Aprili 13, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus imesema kuwa uteuzi huo umeanza mara moja.

Sophia Simba aliyezaliwa Julai 27, 1950, ni mwanasiasa wa kutoka CCM aliyeshika nyadhifa mbalimbali katika chama hicho na Serikalini.

Kitaaluma ni mwanasheria aliyepata elimu yake katika chuo Kikuu cha Dar es Dar es Salaam na baadaye Chuo kikuu cha Zimbabwe.


 
Aliwahi kuwa diwani na baadaye akawa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) nafasi iliyomwezesha kuwa Mbunge wa Viti Maaluma.

Kutokana na ubung wake, aliteuliwa kuwa wazitika wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto na baadaye Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais- Tume ya Utumishi wa umma na Utawala Bora.

Machi 2017 alifukuzwa ndani ya CCM na waliokuwa viongozi wengine kwa madai ya usaliti ndani ya chama hicho. Hata hivyo, Novemba 2017 alirejeshwa baada ya kuomba radhi.


Katika hatua nyingine, Rais Samia pia amemteua Jaji Hamisa Hamisi Kalombola kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma.

Jaji Kalombola ni Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Pia, Taarifa hiyo imesema kuwa Mkuu huyo wa nchi amemteua pia Obey Nkya Assery kuwa Mwenyikiti wa Bodi ya Usimamizi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC).

Assery ni Mshauri Mwandamizi, Taasisi ya Global Alliance for Improved Nutrition, Dar es Salaam.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad