Rais Samia Suluhu Hassan
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema heshima ya utumishi wa umma iliyokuzwa katika awamu ya tano ilikuwa ya woga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumamosi tarehe 2 Aprili Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi wateule.
“Hali yetu ndani ya civil service si nzuri sana, tunasifiwa kwamba adjustments tulizofanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima, lakini heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwasababu kulikuwa na Simba wa Yuda ambaye ukimgusa sharubu anakurarua hata hivyo haijakua vizuri, ” Rais Samia
Mkuu huyo wa nchi amesema heshima inayotakiwa “iwe ya moyoni kila mmoja awe na itikadi moyoni kwake kwamba mimi ni mtumishi wa Serikali majukumu yangu ni haya.”
Aidha amewataka kila mytumishi kuheshimu mipaka yake na kuepuka kuingilia mipaka ya mwingine, “kila mmoja aheshimu line ya mwenzie. Hicho tunakosa Serikalini.
“Unaangalia leo kila siku unasikia Waziri kaparurana na Katibu, Naibu hamuheshimu Waziri wake sijui nani kafanya nini, nafikiri kuna kitu tunakosa pahala.”
Amesema kutokana na hali hiyo kwa upande wa Serikali inakwenda kuimarisha chuo cha utumishi na chuo cha uongozi ili kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma nchini.