Rais Samia Awafuta kazi M/kiti, Bosi MSD



RAIS Samia Suluhu Hassan amemfuta kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) siku kadhaa baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kubaini bohari hiyo ilishikilia zaidi ya Sh Bilioni 14 za hospitali kwa mwaka mzima bila kupeleka madawa na vifaa tiba.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus jijini Washington, DC Marekani, Rais Samia amemteua Afisa Mwandamizi katika Kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PwC) Bi. Rosemary Slaa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bohari ya Dawa.

Pia amemteua Kiongozi Mkuu wa Mradi wa USAID Global Health Supply Chain Technical Assistance Bw. Mavere Tukai  kuwa Kiongozi Mkuu wa MSD.

Bohari Kuu ya Dawa MSD ililipwa Sh bilioni 14.1 kwa ajili ya kununua dawa na vifaa tiba za hospital za rufaa 27, hata hivyo ilishikilia fedha hizo bila kupeleka dawa na vifaa tiba kwa zaidi ya mwaka mmoja, Hali hii ilisababisha uhaba wa dawa na vifaa tiba kwa zaidi ya mwaka mmoja katika hospitali na kukwamisha utoaji Huduma”


 
“Ninapendekeza MSD ipeleke Madawa na vifaa tiba katika hospitali za rufaa husika ili ziweze kutoa huduma za Afya kwa wananchi,’’ alisema CAG, Charles Kichere.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad