Rais wa Ukraine Aambia Ulimwengu Kujiandaa kwa Urusi Kutumia Silaha za Nyuklia Muda Wowote Kuanzia Sasa



 
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonya kuwa Urusi huenda ikatumia silaha za nyuklia katika uvamizi wake nchini Ukraine
Zelensky ameutaka ulimwengu kuwa tayari kukabiliana na unyama wa Rais wa Urusi Vladimir Putin ambaye amemtaja kuwa mtu asiyethamini maisha ya raia wa Ukraine
Mnamo Februari 27, Putin aliamuru Jeshi la Ulinzi la Urusi kuweka tayari vikosi vyake vya nyuklia akidai kuwa vikwazo dhidi ya taifa lake kuwa chanzo
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky sasa anautaka ulimwengu kujiandaa kwa kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin anaweza kutumia silaha za nyuklia katika vita nchini Ukraine.

Rais wa Ukraine Aambia Ulimwengu Kujiandaa kwa Urusi Kutumia Silaha za Nyuklia Muda Wowote Kuanzia Sasa
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (kulia) na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin.
Katika mahojiano na runinga ya CNN mnamo Ijumaa, Aprili 15, Zelensky alisema kuwa kuna uwezekano wa Putin kuchukua uamuzi huo kwa kuwa hathamini maisha ya raia wa Ukraine.

“Sio mimi tu, bali dunia nzima. Mataifa yote yanastahili kuhofia kwa sababu hauwezi kuwa uongo, bali ukweli tu. Silaha za kemikali wananaweza kutumia kwa sababu kwao maisha ya watu hayana maana,” Zelensky alisema.

DP Ruto Ashuku Usajili wa Laini za Simu Una Njama Fiche Inayohusiana na Uchaguzi
Rais huyu aliutaka ulimwengu kuwa tayari kwa chochote kutoka kwa utawala wa Moscow akidai kuwa mataifa mengine hayafai kuopga bali yanastahili kuwa tayari kukabiliana na Putin.


 
“Hatufai kuogopa, tunafaa kuwa tayari. Hili sio swala la Ukraine tu, bali swala la ulimwengu mzima,” rais huyo aliongeza.

Putin aweka tayari vikosi vya nyuklia
Mnamo Februari 27, Putin aliamuru Jeshi la Ulinzi la Urusi kuweka tayari vikosi vyake vya nyuklia siku chache baada ya taifa hilo kuvamia Ukraine.

Putin alisema hatua yake ni kufuatia matamshi ya uchokozi yaliyotolewa na viongozi wa muungano wa NATO na kuwekea Moscow vikwazo vya kiuchumi.


"Kwa sababu hii, ninaamuru waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi kuweka vikosi vya nyuklia katika kazi maalum ya mapigano," alisema kama alivyonukuliwa na Sky News.

Hatua hiyo iliripotiwa kuziweka nchi za Magharibi katika hali ya tahadhari huku vita vya Urusi na Ukraine vikiendelea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad