Waziri wa Nishati, January Makamba amesimama Bungeni na kujibu hoja za Wabunge kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta ambapo amesema Serikali inafanya mazungumzo na nchi wauzaji na wazalishaji wa mafuta ili kupata nafuu ya bei katika kipindi hiki.
Makamba ametoa kauli hiyo wakati wa kuhitimisha mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu kwa mwaka wa fedha 2022/23
“Mwenendo wa bei ya mafuta kwa miezi 16 kwa muda mrefu tumekuwa na ndoto ya kuhifadhi ya kitaifa ya kimkakati ya mafuta hatimaye mwaka huu ndoto hiyo itatimia tunaandika kanuni za kuiwezesha kuwepo vilevile tumepata washirika katika uwekezaji wa miundombinu ya ushushaji na uhifadhi wa mafuta ili kuwezesha hifadhi hiyo kufanyakazi lakini ndani ya serikali tumezungumza kuhusu kuanzisha mfuko wa kuhimili ukali wa bei ya mafuta ambayo katika siku zijazo itasaidia kutuokoa katika nyakati kama hizi, tunaendelea na mazungumzo na wauzaji na wazalishaji wa mafuta ili tuone kama tunaweza kupata nafuu katika kipindi hiki“