Sakata la Watumishi wa Darasa la Saba Laibuka Bungeni


Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Deogratius Ndejembi akijibu maswali bungeni leo Jumatatu Aprili 10, 2022. Picha na Said Khamis
New Content Item (1)By Sharon Sauwa
Dodoma. Watumishi wa umma 1,191 walioajiriwa wakiwa na elimu ya darasa la saba kabla ya mwaka 2004, ambao walikuwa hawajajiendeleza kitaaluma wanatakiwa kulipwa michango yao ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

Hayo yamesema leo Jumatatu Aprili 11, 2022 na Naibu wa Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Arumeru Magharibi (CCM), Lembris Noah.

Noah amesema kulikuwa na watumishi wa darasa la saba ambao walisimamishwa.

“Na wamefanya kazi kwa muda mrefu na baadaye hawakupewa kiinua mgongo wala chochote Serikali inatoa kauli gani kuhusu watumishi hao waliotumikia Serikali kwa muda mrefu?


Akijibu swali hilo, Ndejembe amesema kuwa serikali imeshatoa tamko kwa watumishi wa darasa la saba walioajiriwa kabla ya Mei, 2004 lakini hawakugushi vyeti vyao.

Amesema watumishi hao walipewa muda hadi kufikia Desemba 2020 wawe wamejiendeleza na waendelee na ajira zao.

Amesema kwa wale ambao hawajajiendeleza hadi kufikia muda huo Serikali ilitaka walipwe michango yao ya hifadhi ya jamii.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad